|
SWALI:
Nini hukumu ya mwenye hedhi na mwenye nifasi kusoma Qur-ani kwa
kutazama na kwa kuhifadhi katika hali ya dharura, kama vile yeye kuwa
ni mwanafunzi au mwalimu?
JIBU:
Si vibaya/dhambi kwa mwenye hedhi au mwenye nifasi kusoma Qur-ani
ikiwa ni haja/dharura, kama ilivyo kwa mwanamke mwalimu au
mwanafunzi. Au yule anaye soma uradi wake wa usiku/mchana ambao ndani
yake mna aya za Qur-ani. Ama kusoma Qur-ani kwa ajili ya kupata
ujira/thawabu za usomaji wa Qur-ani, lililo bora mno ni kuacha
kusoma, kwa sababu wengi wa wanazuoni wanaona kwamba si halali kwa
mwenye hedhi kusoma Qur-ani.
Allah
ndiye Mjuzi mno.
|