|
|
| |
MASWALI
NA MAJIBU-Ndoa na Talaka |
| |
|
| Ndoa
na Talaka-Sehemu
ya Nne |
|
|
|
|
|
- Salaam
Aleikum, mimi ni mke mwenye watoto 6 naishi
ulaya.Kuwa na watoto wengi huku ni shida
sana hivyo kwa bahati sasa hivi nimepata
mimba na ni changa bado, je sheria
inaniruhusu kuitoa?kwani huwa nadhoofika
sana kiafya na siwezi kupata mtu wa
kunisaidia kuwatunza watoto tena ni wadogo
sana na Baba yao anafanya kazi.
- Mimi
ni Mke wa Mtu na nina watoto 6 na naishi
huku Ulaya mama yangu ni mgonjwa huko Afrika
hata mimi nimgonjwa na nataka kusafiri
kwenda kumuona jee, naruhusiwa kusafiri peke
yangu bila ya mume wangu? kwani gharama ya
nauli kwa familia yangu yote ni kubwa sana!
- je
uislamu unaruhusu baba na mtoto wake kuowa
mtu na ndugu yake
- swali,
nina ndugu yangu ambaye alizaa na mwanamke
bila kufunga ndoa, kwa bahati huyo ndugu
yangu umri wake ukaisha yaani mwenyezi mungu
amemchukua (amefariki. sasa baadhi ya ndugu
wanataka yule mtoto aliyekuwa amezaa nje ya
ndoa marehemu akombolewe ili awe mtoto
aliachwa na marehemu.je inawezekana,kisheria
ya dini inakuwaje
- je
msichana wa kiislamu akiolewa aweza kukata
uhisiano wa wazazi wake au ndugu zake
- mimi
ni muislam , nimezaliwa
katika uislam,
nimeoa, lakini mke wangu
alikwenda mji mwengine
kutafuta maisha, ili
halafu mimi nimfate,,,
lakini uwezo wa mimi
kumfata ni mgumu kwani
yuko mashariki ya mbali,
sasa ni muda wa
miaka 5, au sita na
anadai hanitaki tena si
mke wake, na
mimi nampenda nikaoa mke
mwengine na huku bado
namtegemea yeye arejee
turudi kama mke na
mume, je ? unanishauri
ni ni? ni muache,
au akirejea ni mke
wangu, au nitoe talaka,?
nategemea zaidi toka
kwako,,,maasalam,
- IKIWA
MUME NA MKE WANAISHI NYUMBA MOJA LAKINI
KILAMTU NA CHUMBA CHAKE KWA MUDA WA MIAKA 5,
MUME HAWEZI KULALA NA MKEWE NA MKE
AMEVUMILIA SANA ANAHAKI YA KUOMBA TALAKA (INAMJUZIA
MWANAMKE KUOMBA TALAKA.)
- Je,
mwanamke(muislam)anaruhusika kuzuru makaburi
ili kuombea dua maiti?
- swali
nauliza mimi ninamwanangu anataka kuolewa na
nimetoa idhini kwa mtu mwengine amuoze mume
mwanangu na mimi nipo hapohapo je inafaa au
haifaa sababu wengine wanasema inafaa
wengine wanasema haifai je jibu sahihi
nilipi?
- Swali:mimi nina mke na mtoto,na nilikubaliana na mke wangu kuhusu swala
la kutafuta maisha na sasa nikombali na yeye
kwa muda wa miaka miwili,Alhamdulillahi
tunawasiliana kwa simu na vilevile nnamtumia
hela kila baada ya wiki mbili,sasa kumetokea
mtu kaniambia ya kwamba kuna miezi imewekwa
kwenye dini ikiwa hujamuingilia mkeo kwa mda
wa miezi mnne unakuwa umeshaachana naye,
je,mada hii nikweli na kama nikweli
nifanyeje? kwani kuna malengo ambayo
tumeyapanga mimi na yeye mke wangu na bado
hatuja yafikia na bado itachukuwa mda wa
mwaka mwengine.
JIBU
Rudi
Nyuma
Endelea
Mbele
|
|
|
|
|
|
| |
|
|
| Tuandikie |
| |
|