|
|
| |
MASWALI
NA MAJIBU-Ndoa na Talaka |
| |
|
| Ndoa
na Talaka-Sehemu
ya Tatu |
|
|
|
|
|
- Je
inakubalika kisheria kwa mwanaume mwenye mke
kuoa mke mwingine bila kumtaarifu mkewe?
Kama inakubalika kisheria zamu zinawezekana
kupangika bila mke mkubwa kujua? Naomba
ufafanuzi.
- swali
langu kuhusu baadhi ya Mashekh wanasema
kwamba baina ya mwanamume na mwanamke
wanapozini kwani wengine usema yafaa kuoana
wengine wanasema kwamba haifai lipo jibu la
kweli kwani ktk kupita kwangu nimeona watu
wazaa na wamejuku baada ya Kurudi
Makka wameachana kwamba wameambiwa wanaishi
kwa haramu vipi kuhusu wale watoto tuseme ni
wa haram? basi kuhusu itakuwa familia yote
ya haramu
- Suala:
Jee inafaa mwanamke aliye na hedhi :
1- kujitia hina kichwani (nweleni)?
2- kukata kucha?
3- kutoa malaika (nwele) miguuni, mikononi,
kwapani?
4 - jee, inafaa vile vile kutowa nyusi ikiwa
nyusi zake zimetambaa sana, na nyingi.
- Mwanamke
ana hedh, inafaa kuvaa kidani chenye aya za
kuraani, au jina la Mwenye Enzi Mungu?
Inafaa kusoma Quraan kwa sauti sura
ulizohifadhi? ukiwa na hedhi?
- Kawaida
ya hedhi yangu ni siku 5.
mara hii imemalizika kama kawaida siku ya
tano, nikakosha nikatia tohara, nikasali,
lakini siku ya sita kuingia ya saba ikatokea
tena damu kidogo pamoja na rangi rangi ya
chockleti(brown).
Jee, nini hukumu yake? niendelee
kusali na faridha za kawaida au nikoge, na
nitie tena tohara?
- Mimi
naishi Ulaya, nina mke na watoto 4. Huku
ulaya ukiwa na watoto wengi unapata matatizo
mengi kama vile kulipa kodi nyingi
serikalini na mtu unakuwa kichekesho mbele
ya jumuia na kuonekana punguani na unaweza
kupokonywa baadhi ya watoto wako na serikali.
Sasa mimi kwa hofu hiyo huwa natumia kondom
ninapoingiliana na mke wangu ili kuepuka
kuzaa zaidi na kuoa mke mwingine sheria za
huku haziruhusu, jee, sheria inaruhusu hayo?
- A.
Mimi najua TALAKA ziko 3. Sasa, Ikiwa
mwanamke humtaki kabisa tena na wala
hutarajii kumrejea kutokana na vitimbwi
vyake, na hujawahi kumpa talaka hata moja:
Je, Waweza kumpa talaka 3 kwa mpigo?. (Mf.
kuanzia sasa sio mke wangu x3) ili itimie
talaka 3?
B. Ukimpa talaka 3 bado anastahiki
kuisubiria eda yake nyumbani kwa Mumealiye
mtaliki?.
- mimi
nauliza hivi mimi kwa sasa niko
england lakni nimepata
jambo moja huku england haturuhusiwi
kuwa na wake wawili sasa na mimi
nilikuwa nataka kuoa mke wa huku
engalnd na wakati huo nilikua na
mke tanzania tayari ikabidi nimuombe
mke wangu wa huko tanzania
anitafutie karatasi zinazoonyesha kama
nimemuacha lakini mimi sijamuacha kwa mdomo
wala kwa maandishi na mke wangu
ameenda mpaka mahakamani
kunifanyia hizo karatasi ili niweze
kupata sheria ya huku je shekh
nauliza mimi sijamuacha mke wangu je
watu wansema hiyo itakua imesihi
kuwa talaka wakati mimi sijamtamkia wala
sina nia ya kumuacha je shekh nitakua
niko katika sehemu gani nimewacha mke
au sijawacha
- Kwa
kuanza ninaanza na swali langu kuwa mtu
ukioa halafu yule mwanamke akawa anatii
maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na
kutonisikiliza mimi kila ninalomwelewesha je
ni haki kumpa talaka?
- Napeenda kuuulizwa swali. eti kama mtu unaoa na ni mjamzito eti kweli
ndoa inasihi. Na alafu mimi nataka kuoa bila
ya wazee wangu kujuwa kweli ndoa yangi
itasihi?na swala la mwisho eti kama nitakuwa
na mwanamke wa kikiristo na nitaamua
kumsilimisha na kuingia katika dini ya
Kislam. na nitafunga naye ndoa itasihi?
wakati kabla nimeshatembea nae na
nimeshapata naye mtoto mmoja. Naomba majibu
ya maswala haya ili nielewe
JIBU
Rudi
Nyuma
Endelea
Mbele
|
|
|
|
|
|
| |
|
|
| Tuandikie |
| |
|