-
Mimi ninamke
wangu wa ndoa, na nimepata nae watoto. Baada
ya makubaliano ya kutafuta maisha tukaamua
nisafiri niende mbali ya nchi kwa kutafuta
maisha ninawashughulikia kwa kila hali na
kuwakidhi kimaisha ila tu ni muda mrefu sasa
hatujaonana kwa tendo la ndoa. Suala
langu:- Baada
ya muda kupita mkewangu alinilazimisha kuwa
wakati ni mkubwa na hawezi tena kuvumilia ni
afadhali nirejee nyumbani kwa kweli hadi hii
leo sijapata uwezo wa kurudi.
1.
Jee
mwanamke huyu akibeba mimba na kuzaa mtoto
jukumu hili litakuwa kwa nani?
2.
Ikiwa
atafanya mambo ya zinaa jukumu hili ni kwanani?
3.
Na
ikiwa anatoka ndani ya nyumba yake bila amri
yangu nani atachukua jukumu hili?
4.
Mwanamke
huyu hatokuwa na mchunga kwa muda wote huo jee
mimi sitokuwa ni mas-ul juu ya hali hii.
Ninakuomba unitatulie matatizo yangu kuwa hapa ni njia tu nahovia maisha ya
baadae.
- MARA
NYINGI HUTOKEA KUTOELEWANA KWA KUMALIZA EDA
YA MWENYE KUFILIWA NA MUME.SASA VIPI EDA YAKE HUISABIWA KWA MIEZI YA KIISLAMU
AU YA KIKRISTO (KIZUNGU)KAMA JAMII
ILIVYOZOEA??
- MTU
ANA MKE WAKE WAMEISHI MIAKA KADHAA GHAFLA
MKE AKADAI TALAKA MUME HAKUTAKA KUMUACHA,
MKE AKAENDA KWA KADHI NA MUME AKAITWA KWA
KADHI, NA BADO MUME AKAGOMA KUTOWA TALAKA
KWA MAMLAKA ALIYOPEWA KADHI AKAMUACHA MKE
YULE BILA MUME KURIDHIKA NA MKE AKARUDI
NYUMBANI KWAO KWA SABABU KESHA ACHWA NA MUME
ANASEMA YULE BADO NI MKEWE KWA SABABU
HAJAMUACHA, SIKU ZIKAPITA MKE AKAKAA KABLA
YA EDA KUMALIZIKA AKABADILI MAWAZO AKATAKA
KURUDI KWA MUME WAKE JEE MUME YULE ATAMPOKEA
KAMA NI MKEWE KWA SABABU ANASEMA HAJAMUACHA
AMA AMREJEE.
- swali
langu kama mzazi ambaye hajatoka arobaini
anaruhusika kuchezeana na mumewe?au si
vizuri kufanya hivyo.
- kwa
nini wanaume wa kiislam wamekubaliwa kuoa
wake wanne?
- Mimi
ni mwanamke wa kislam na nilikutana na
mwanamme ambae si mwislam ila baba yake ni
mwislam na mamake ni mkiristo na amelelewa
katika ukiristo na tumependana nae na
tunataka kuishi wote je, kwanza yeye
atahesabika ni mwislamu au mkristo? Pili
nimemgusia kubadilisha dini amekataa je,
itafaa kufunga nae ndoa ya serikali?
- JE
NDOA INASIHI KUFUNGISHWA NA MWANAMKE AMBAYE
YUKO KTKA SIKU ZAKE(HEDHI)?
NA KAMA INAKUBALIKA VIPI SASA USTAHMILIVU WA
MUME KWA MKEWE WAKATI YUKO KTKA HEDHI
NA KWANZA NDIO WAMEOANA?
- mimi
nimeoa hivi juzi sasa vipi haya madhii huwa
yananitoka pasi kutarajia na kwa siku
hunilazimu kubadilisha nguo zaidi ya mara
moja sasa naona kuwa ni kero je kuna njia
nyengine ili niondokane na usumbufu huu ? au
ninasamehewa na sheriya kwenda kusali hivyo
hivyo??
- mimi
nina mume nilieozeshwa na wazee wangu, sasa
ni miaka mingi hatuna uhusiano wa kindoa
lakini tunaishi katika nyumba moja na
nishawahi kumwambia ni bora ya kuachana
lakini naona hana fikra hiyo, nini ushauri
wenu, tafadhali hili linanitatiza sana.
- swala langu ni hili nataka kujua katika uislam na ndowa ipo contract ya
mume na mke ikiwa mwanamke anataka kuolewa
akampa msharti huyo mwanamme nini anataka
nini hataki jee inafaa
JIBU
Rudi
Nyuma
Endelea
Mbele
|