|
|
|
|
|
| Ndoa
na Talaka -Sehemu
ya Tano |
|
|
|
|
|
- Mimi
nilikuwa Muislamu na nimeolewa na mtu
sio muislamu na sasa nimebadilisha dini,
nimekuwa jewish. Je kuna tatizo mbele ya Mwe/M.
Mimi ninachojua katika Uislamu haifai
mwanamke kumbadilisha mwanaume kuingia
katika dini nyingine. Kama upo uwezekano
naomba uniambie.
- Jee,
hali mke anaweza kumkatalia mumewe kukhusu
maingiliano yao ya kijinsi,kwa sababu za mke
kutaka kufanya ibada, kama kufunga,kusali
suna au haja ya kusoma tasbeeh au
qur-aan,baada ya fardhi??
- mimi
nilikuwa nina swali kwamba kama mtu ameoa
baada ya hapo Mwenyezi Mungu akawajaalia
mtoto sasa yule mwanaume anapaswa amuingilie
mke wake baada ya muda gani hapo uislam
unatuelezaje? na hapo hapo atakapomuingilia
kuna dua gani inasomwa na jingine kwa
kuongezea kwenye mada hii muislam
unapomuingilia mke wako huwa kuna dua ambayo
unasema ya Mwenyezi Mungu awajaalie kile
kiumbe kitakachokuja kiwe miongoni mwa mja
ambaye anatekeleza maamrisho ya Mwenyezi
Mungu sasa basi kama huyo muislam
anamuingilia mke pasina kutaka mtoto ni kwa
ajili ya kukidhi haja zake je hapo
kuna dua gani inayosomwa? inshallah yangu ni
hayo kama kuna mahala nimekosea naomba radhi
binadamu ndio mkoseaji,
- Mimi
ninabinti nataka kumuoa lakini kuna suala
bado linanipa utata.
1. Binti huyo alishaolewa miaka minne
iliyopita huko nyumbani.
2.Mara baada ya kuolewa alikaa siku chache
kisha aliondoka kuja huku ulaya kwa masomo
3. alikuwa akiwasiliana na mumewe kwa kwa
kipindi cha mwaka mmoja na nusu.
4.Baaada ya hapo akapata habari kwamba
mumewe anafanya uzinifu na kazaa na mwanamke
mwingine.
5.cha kutatanisha zaidi mume huyo alikuwa
mkristo kabla hawajaoana alibadili dini ili
aweze kumuoa binti huyo.
6.sasa hivi huyo bwana karudi kwenye ukristo
na hakuna mawasiliano kati yao.
SWALI NI HIVI NINAWEZA KUMUOA HUYU BINTI
INGAWA HAJAPEWA TALAKA? AU NINI NIFANYE ILI
NIWEZA KUMUOA BINTI HUYU.
- a-ni
nani anayefaa kuozesha?
b-je mtu ambaye hana mke na hajawahi kuoa
anafaa kuozesha?
- MWANAMKE
ALIKUWA AKIISHI NA MUMEWE NA WATOTO WAKE NA
MDOGOWAKE WAKIKE, MARA YULE NDUGU AKASHIKA
MIMBA ALIPO ULIZWA NA DADAAKE AKASEMA ALIYE
NITIA MIMBA HII NI MUMEO YAANI
SHEMEJIYAKEALIYE NDANI YA
NYUMBA.AKAJIFUNGUWA NA MTOTO AKATOLEWA DAMU
NI DAMU YA MUMEWE SAWA.AMEPATA USHAHIDI
KAMILI.
INAJUZU HUYU MWANAMKE KUENDELEA KUISHI
NA MUMEWE KI MKE NA MUME?
- IKIWA
MKE ANAISHI KATIKA NCHI ZA UARABUNI NA MUME
ALIKWENDA AFRICA KWA AJILI YA MATIBABU, HUKO
HUKO AKAFARIKI DUNIA.ILIPOKUJA KHABARI YA
MUME AMEFARIKI, MKE AKATAKA KWENDA KUMZIKA
MUMEWE PAMOJA NA WATOTO WAKE (MUHRIMU ZAKE)
BAADHI YA MASHEKHE WAKAMWAMBIA HAIJUZU
KUTOKA KWENYE NYUMBA YAKO, WENGINE
WAKAMWAMBIA UNAWEZA UKATOKA LAKINI MAGHARIBI
UWE UMEISHA FIKA, NA WENGINE
WAKAMWAMBIA UNAWEZA UKASAFIRI MADHALI NA
WATOTO WAKO WAKIUME WOTE.
SASA SUALA LANGU INAJUZU KUSAFIRI KWANI
ALIKUWA ANAWAHI MAZIKO HUKO ANAKO KWENDA.
- NANI
ATAKAYE WEZA KUTOWA IDHINI YA KUOLEWA KWA
MTOTO ULIYE MLEA.
IKIWA MIMI NA MUMEWANGU TUMECHUKUWA WATOTO
HOSPITAL TUKAWALEA MPAKA UMRI WA KUPEWA
WAUME, IMETOKEA RISKI YA WACHUMBA KUJA
KUWAPOSA SASA WATOTO HAWA ITATUJUUZIA SISI
WALEZI KUTOWA IDHIN YA KUOLEWA AU ITABIDI
IDHIN ITOKE MAHAKAMANI?
- suali
langu ni ikiwa mwanamke anataka aachwe na
mumewe kwa sababu ya kuto enjoy na huyo mume
na hawezi kumwambia kama amuache,wakati huyo
mume hana tatizo lolote, tatizo ni huyo m/ke
ndio anajilazimisha tu kuishi na huyo
mumewe,sasa kama kuna DUA yoyote ya kumuomba
Allah ili iwezekane KUACHWA basi tunaomba
tufahamishwe,kwani huyo m/ke anaona pia
anapata dhambi kwani hana hamu hata ya kukaa
na mumuwe,na anaona dhiki ktk
maisha yake kwa kuishi tu na mtu ambaye hana
mapenzi naye, na wala hamvutii,ni anaishi tu
kama hana budi na anampenda kama kawaida tu
sio kama mke inavyotakiwa kumpenda mume.basi
tunaomba msaada
- Suala langu ni kuhusu kurithi kwa watoto mali ya
mama yao aliyefikwa na mauti. Je iwapo kuna
mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa na ana ndugu
waliozaliwa ndani ya ndoa, watagawana
vipi mali ilyoachwa na mama yao? Kwa mfano
iwapo watoto ni watatu na wote wa kiume.
mmoja wa hao ni mtoto wa nje ya ndoa.
Je watagawana kama ilivyo kawaida ya
urithi wowote au huyu mwana nje kwa kuwa
hana haki kwa baba atapata zaidi
JIBU
Rudi
Nyuma Endelea
Mbele
|
|
|
|
|
|
| |
|
|
| Tuandikie |
| |
|