|
|
| |
MASWALI
NA MAJIBU-Masuala mengine ya Dini |
| |
|
| Masuala
mengine ya Dini -Sehemu
ya Pili |
|
|
|
|
|
- Maswali
yangu leo nayajenga kutoka katika Qur'ani
5:5,9:28, na 9:95.
Kwa muktasari Allah katika surat(Al-Maida
5:5) anasema:
--Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali
kwenu,
--na chakula chenu ni halali kwao. .......)
Pia Katika surat (Tawba 9:28/95) anasema:
Katika Aya 28.Enyi mlio amini! Hakika
washirikina ni najsi, .......)
na Katika Aya 95. ......Hakika hao ni najsi,
na makaazi yao ni
Jahannamu,........)
MASWALI:
(1).Je, Washirikina hao kwa sasa ni akina
nani? kati ya (Mayahudi,Wakristo
na wengine mf. Mabaniani).?
(2).Ni daraja gani hadi mtu aitwe kuwa 'mshirikina'?,
ikiwa Ushirikina ni
kuabudu kitu chochote kinyume na
Mwenyenyezi-Mungu kama vile kuabudu
(sanamu, ng'ombe, mtu, na Mitume wa Allah
n.k): Sasa Je, anayemuabudu
mtu/Mtume (yaani Mayahudi/Wakristo) kumfanya
ni mungu, na anayeabudu sanamu
au ng'ombe kumfanya ni mungu; Ni nani
mshirikina haswa kati ya makundi haya
mawili????.
(3).Je, watu wakitabu hao ambao tule kwao
kwa sasa ni wapi? na ibada zao
wanazifanyia wapi? na wao wanaitikadi gani
ya kuhusu Allah ni Mmoja?.
(4).Je, ni aina gani ya chakula ambacho ni
kharamu kula kwa washirikina (au
hata soda, biskuti, embe nk.)? Maana huku
maofisini ni mtihani, wananunuaga
vitu kama soda, chips n.k halafu kisha
twakaribishana sasa je, vipi
hapo!!!!? (Ambao ni Mabaniani wanao abudu
ng'ombe).
(5).Je, kwakuwa wao ni najisi, itakuwaje
baada ya kuchuwa Udhu wako barabara
kisha ukagusana naye udhu wako utatenguka?
Au Je, akigusa chakula
ulichopanga kukila kitanajisika?
(6).Akikupa zawadi kama Fedha, Nguo, Redio
n.k usichuwe?
- Baada
ya kufa Mtume muhammad kulikua na makhalifa
wanne ambao wakiongoza dini hii ya kiislamu
yaani Othmani, Abubakkar, aLY na Omar.
Wakati wa uongozi wao waislamu walikuwa
wakiwasikiliza, kuwaamini na kupanga mambo
yao kua kitu kimoja. lakini baada ya kufa
wao hivi sasa waislamu hatuna kiongozi hata
mmoja anaetuunganisha katika dunia hii chini
ya uislamu. Tunaamini kitabu cha allah
kinatusaidia kutoungoza.
Swali Jee dini inatukataza kuwa na
kiongozi wa kiislamu katika dunia hii ili
tuwewamoja?
Kitu gani kinatukwamisha sisi waislamu kuwa
na kiongozi mmoja wa kislamu ili tuwashinde
adui zetu chini ya ulimwengu huu?
- suala
langu ni nataka kujua mama yake mtume s.a.w
alipokufa alikufa muislam au la pamoja na
ami yake aliyemlea.
- tulisoma
kwamba mwenyezimungu ana sifa ya kuongea kwa
ushahidi kwamba aliongea na nabii Musa (a.s)..na
maneno ya Allah hayana herufi wala sauti ..sasa
basi naomba nifahamishwe vipi nabii
Musa(a.s)alijua kama mola sasa anamtaka avue
viatu ktk lile jangwa takatifu ....hali ya
kuwa maneno yake mola hayana sauti wala
herufi ?????
- Kutokana
na Aya hiyo hapo chini ya (Surat Hajj
22:40): Allah Aliposema:
. Wale ambao wametolewa majumbani mwao
pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola
wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa
Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi
hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za
wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na
misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi
Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka
Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia
Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu
Mtukufu.
---------------
(1)Je, ni watawa gani hao ambao
wanaokusudiwa?, (inamaana ni masister na
mapadre?). Na je, wanalitaja namna gani hilo
jina la Allah?, (Au ndio zile nyimbo zao na
matarumbeta)?
(2)Je, Hayo masinagogi ni yapi?
(3)Je, makanisani napo. WANALITAJA VIPI jina
la ALLAH? (Au ni makanisa yapi hayo?)
-------------
Mimi nimeuliza maswali haya, hii yote
nikutokana na mkristo mmoja, alinijia
akanipa hii aya kisha akadai kwamba: Jina la
Mwenyezi Mungu linatajwa kanisani halafu
nyinyi mnasema ukristo sio dini vipi, mbona
Muhammadi wenu anakudanganyeni?). Wallahi
mimi nilishindwa jinsi gani nimjibu ili
anielewe, nikakaa kimya. Na ndio mara yangu
ya kwanza kuiona aya hii.
Sasa nakuombeni munisaidie kwamba Allah
aliposema hivyo ki-elimu amekusudia nini?,
Watawa gani?, makanisa gani?, masinagogi
gani?.
- SUALA
LANGU NIKIOMBA KUULIZA IKIWA MTU AMEOKOTA
PESA NJIANI KATIKA MJI WA SAUDIA,
AMEISHA MALIZA KUFANYA HIJA YAKE, ANARUDI
KATIKA MJI WAKE. PAHALA HAPO HAPANA MAJUMBA
KUNA PETROL STATION TU. JE ZINAMHALALIKIYA
PESA ZILE KUZITUMIYA NAOMBA MNIFAFANULIYE.
BI TAUFFIQ.
- Je!
Inajuzu Kisharia Kulijengea Kaburi La
Muislamu Kwa Saruji (Cement) Na Kuandika
Jina Au Tarehe Au Hata Baadhi Ya Aya Za
Quraan Juu Ya Kaburi Hilo? Ikiwa Jambo Hilo
Halijuzu. Inajuzu Kubomoa Kaburi Baada Ya
Kujengewa Kwa Saruji (Cement)? Tafadhali
Naomba Ufafanuzi Na Jibu la yakini Ambalo
Halina Shaka Katika Swala Hili muhimu.
- 1-
IKIWA MZAZI YUHAI ALIWASIA
NIKIJA KUFA MTOTO WANGU ASILIGUSE
JENEZA LANGU,KWA SABABU AMEOLEWA NA MUME
MKIRISTO. JE INAMAANA YULE MTOTO AKIENDA
KULIBUSU JENEZA LA MZEE WAKE. ITAKUWA NI
HARAMU KWAKE.
- TUNAVYO
JUWA KUMNYONYESHA MTOTO MAZIWA YA KIFUANI
MTOTO ALIYEKUWA SI WAKO INAKUWA NA WATOTO
WAKO WASHAKUWA NDUGU HAWAWEZI KUOWANA.
JE MWANAMME AKATOWA DAMU KUTIWA
MTOTO WA KIKE ALIYE KUWA SI DADA YAKE
INAMJUZIA KUMUOWA?
- swali langu ni kuku wanaochinjwa na wayahudi [jews] sisi waislam
tunaruhusiwa kula?maana yake wengine
wanasema wanafaa na wengine wanasema maadamu
hakuna kalima iliyosemwa wakati wa kuchinja
basi basi hawafai-tuondolee mushkeli sheikh
kwa sababu sisi tunaishi ugenini huku
JIBU
Rudi
Nyuma
Endelea
Mbele
|
|
|
|
|
|
| |
|
|
| Tuandikie |
| |
|