KUMTOA NJE BI. HARUSI (HADHARANI)
BI. HARUSI KUVIKWA SHELA
Ndoa ni suala nyeti kabisa katika
maisha ya mwanadamu. Unyeti wa suala hili la ndoa unajidhihirisha kutokana na umuhimu wa
ndoa katika kuendeleza kizazi cha wanadamu ambalo hili ni tunda kuu la ndoa. Kadhalika
unyeti wa ndoa unatokana na haja tegemezi ya mwanamume kwa mwanamke na mwanamke kwa
mwanamume. Katika hali ya kawaida kimaumbile mwanadamu na mwanamke ni jozi (pair)
tangamano, hii inamaanisha kwamba kila mmoja anamuhitajia mwenziwe ili kukamilika
kimaumbile. Ni kwa kuuzingatia unyeti huu ndipo sheria ikalitawala eneo zima la ndoa,
kabla na baada ya ndoa. Uislamu ukaweka na kupanga taratibu/kanuni na sheria ambazo
muumini ni lazima azifuate katika utekelezaji wa suala zima la ndoa. Sheria/taratibu hizi
huanzia tangu katika ile hatua ya awali kabisa ya uchumba, ambayo hii hutufikisha katika
posa, utoaji wa mahari, ndoa yenyewe ikiwa ni pamoja na sherehe/hafla zinazoambatana na
ndoa na hatimaye kutia nanga katika maisha ya ndoa. Maeneo yote haya tayari yameshaguswa
na kuwekewa sheria na taratibu amazo zimefafanuliwa kiufasaha kabisa na Bwana Mtume
Rehema na Amani zimshukie- kupitia kauli na matendo halisi. Kwa mantiki hii muislamu hana
nafasi ya kujiundia taratibu zake mwenyewe zinazopingana na sheria. Kufanya hivyo ni kosa,
na mtendaji anastahili kubeba mzigo na dhamana ya kosa lake hilo. Tusome, tutafakari na
tuzingatie:
..NA NI NINI KIKO BAADA YA (kuacha) HAKI
ISIPOKUWA UPOTEVU, BASI MNAGEUZWA WAPI ? (10:32)
Baada ya kuwekana sawa kwa utangulizi huo, hebu sasa tuanze
kuizungumzia mada yetu. Pengine tunaweza kujiuliza kwa nini tumeigusa ndoa wakati mada
yetu kuu ni Bi. Harusi? Tumefanya hivyo kwa sababu hatuwezi kumpata na kuwa na Bi harusi
bila kuwepo ndoa, Bi. Harusi ni zao la ndoa. Haya sasa tukiangalie kwa pamoja kipengele
chetu cha kwanza.
(a) KUMTOA HADHARANI BI. HARUSI
Imezoeleka, imekuwa kawaida na mtindo katika jamii zetu kumtoa nje bi.
Harusi baada ya ndoa kufungwa na hili hufanyika mbele ya kadamnasi ya wanamume na
wanawake. Ada hii imeendelea mpaka kufikia hatua ya kuonekana kuwa ina upungufu na
haikukamilika ndoa ambayo imefungwa bila ya Bi. Harusi kutolewa nje na kuonyeshwa
hadharani. Tunasema hivyo ndivyo tunavyofanya katika harusi zetu na tumezoea au kuzoeshwa
hivyo. Lakini je, hayo ndiyo maelekezo na mafundisho ya Uislamu au ni matashi na matamanio
ya nafsi zetu? Tukubali au tukatae, huku ni kupingana na sheria na ni upotevu unaotokanan
na kumfuata shetani mlaaniwa ambaye ni adui yetu mkubwa. Mwenyezi Mungu
Mtukufu anatuasa na kutuamrisha; ENYI MLIOAMINI! INGIENI KATIKA HUKUMU ZA UISLAMU
ZOTE, NA WALA MSIFUATE NYAYO ZA SHETANI, KWA HAKIKA YEYE KWENU NI ADUI DHAHIRI.
(2:208) Kuendeleza mila na ada hii ni kumdhulumu Bwana harusi, ambaye ndiye mwenye haki na
mkewe (Bi. Harusi). Sasa ikiwa yeye ndiye mwenye haki, sisi tunamuonyesha nani uzuri,
kupendeza na mapambo ya mkewe? Ni dhahiri kuwa katika siku hiyo muhimu kabisa katika
maisha ya mwanadamu, Bi. Harusi hupambwa na akapambika na hali halikatazwi na sheria muda
wa kuwa ni mapambo halali yanayokubalika kisheria. Sasa tunapo
|