|
A: HUKUMU YA SWALA KWA
MUJIBU WA QUR-ANI NA SUNNAH
Ewe ndugu yangu mpenzi; hebu kwa msaada wa
Mwenyezi Mungu Mtukufu tuzianze nasaha zetu kwa
kumuomba Mola wetu Mtukufu atuwafikshe na
kutuongoza katika kuijua haki, kuikubali na ksha
kuifuata-Aamiyn Baada ya dua hiyo, hebu sasa
tutazame kwa pamoja natujiulize nini hukumu ya
ibada ya swala ndipo tutafahamu ni ipi nafasi na
hukumu ya mtu asiye swali .
Ndugu yangu mpenzi, elewa na ufahamu kwamba
swali katika sheria ni FARDH yaani WAJIBU. Haya
ni kwa mujibu wa aya chungu mzima za Qur-ani
Tukufu. Hebu tusitafakari kwa pamoja aya hizi
zifuatazo
"…BASI SIMAMISHENI SWALA, KWANI HAKIKA
SWALA. IMEKUWA KWA WAUMINI NI FARDHI ILIYOWEKEWA
WAKATI MAALUM" [4:103]
Ukizingatia aya hii utakuta inaeleza kwa
ufumbulizo na uwazi kabisa kwamba swali ni
FARDHI, tenasi fardhi tu bali ni fardhi
iliyowekewa wakati maalum na Mwenyezi Mungu
Mtukufu kwa waja wake waumini kauli ya Mola
karim Aliposema: "… HAKIKA SWALAKWA
WAUMINI NI FARDHI ILIYOWEKEWA WAKATI MAALUM
" ni ishara na dalili bayana kwamba swala
ndio kielelezo kikubwa cha Imani ya mja. Kwa
maneno mengine tunaweza kusema kuwa hana Imani,
mtu asiyeswali. Ikiwa mtu hana Imani , vipi
unamtazamia kuwa na dini? Hii ndio maana Bwana
Mtume –Rehema na Amani zimshukie akasema:
Mkimuona mtu aizoya Msikiti basi mshudieni kuwa
yuna Imani kauli hii ya Bwana Mtume inazidi
kutuonyesha ukweli usio pingika kwamba swala
ndio nembo na kielelezo kikubwa cha Imani ya
mja. Hebu tuitafakari na aya hii:-
"HIFADHINI (angalieni sana) SWALA (zote
kuziswali) NA (khasa) ILE SWALA YA KATI NA KATI
"[2:238]
Tukilizingatia neno la mwanzo lilotumika
katika aya (HIFADHINI) tukaliweka katika sarufi
ya kiarabu (Arabic Grammar), tutaambiwa na watu
wa fani ya lugha kuwa neno hili ni tendo la
amri. Kwa hivyo basi neno hili (HIFADHINI)
inbamaanisha kuwa suala la kuhifadhi swala ni
amri itokayo kwa Mwenyezi Mungu kuja kwa waja
wake na wala sio ombi. Sasa kama tunakubaliana
na ukweli huu ulio dhahiri kuwa swala ni amri ya
Mola amuamrisha mja wake, je! Huoni kwamba
kuacha swala ni kupinga na kuivunja amri ya
Muumba wako? Avunjaye na kupinga amri ya Bwana
wake hufanywaje na Bwana wake, hasa ukizingatia
kwamba siku zote amri hutoka kwa Mkubwa aliye
kuja juu kwa mdogo aliye chini kama ambavyo ombi
hutoka kwa aliye chini kuja kwa aliye juu. Hebu
jaribu kuwa mkweli, mwanao au mkeo akivunja amri
yako, unakuwaje na unchukua hatua gani? Ukiukir
ukweli huu ndipo utaiona nafasi yako mbele ya
Mola wako wewe usiyetaka kumsujudia Mola wako.
Naam, tumetangulia kusema huko nyuma kwamba
swala ni FARDHI /WAJIBU, hebu sasa tulitazame
neno WAJIBU limeaanishwa vipi na sheria ili
uione nafasi yako wewe usiyeswali. Wataalamu wa
fani ya fiq-hi wamelianisha neno wajibukwa
kusema (WAJIBU/FARDHI ni lile jambo ambalo Allah
ameliwajibisha juu yetu, hulipwa mtu aliye
baleghe (mtu mzima),mwenye akili timamu kwa
kulitenda/kulitekeleza (hilo la wajibu)na
huaadhibiwa kwa kuwacha kulitenda, kama vile
swala, funga na kuwatii wazazi). Hili ndilo
ainisho (definition) sahali la WAJIBU, hebu sasa
lichukuwe aanisho hili uliambatishe na swala,
unafahamu nini? Ikiwa wewe ni mkweli,
uliokulazimu kwa amri ya Mola Muumba wako na
kwamba ukiswali utakuwa umeikubali na kuipokea
kuitekeleza amri ya Mola wako kwa maslahi na
faida ya nafsi yako, hivyo utalipwa thawabu
ambaazo ndizo "Dollar" za kuinunulia
akhera. Kinyume chake ni kwamba kama hukuswali
utakuwa umeipuzana na kuivunja amri ya Molawako
kwa maangamivu na khasara ya nafsi yako
mwenyewe, kwa hivyo utaaadhibiwa kwanza hapa
hapa duniani, kaburini na kesho akhera kama
lilivyothibiti hilo katika hadithi ya Mtume
–Rehema na Amani zimshukie. Tusome kwa
mazingatio: "… NA BILA SHAKA ADHABU YA
AKHERA NI KALI ZAIDI NA IENDELEAYO
SANA"[20:127]
"ANAYEFANYA MEMA ANAJIFANYIA (mwenye)
NAFSI YAKE, NA MWENYE KUTENDA UBAYA NI JUU (ya
nafsi) YAKE NAMOLA WAKO SI DHALIMU KWA WAJA
WAKE."[41:46]
B: NAFASI YA SWALA KATIKA UIISLAM
Katka kuonyesha umuhimu na nafasi ya
swala,Bwana Mtume- Rehema na Amani zimshukie
–ameijaalia swala kuwa inashika nafasi ya pili
katika nguzo tano za uislam "uislamu
umejengwa juu ya nguzo tano: kushuhudia kuwa
hapana Mola apasaye kuabudiwa ila Allah na
Muhammad ni Mtume wa Allah, kusimamisha swala,
kutoazakah, kufunga ramadhani na kuhiji
Makkah-Mukaram" Bukhaariy.
Ukiitafakari hadithi hii utaona ya kwamba
Mtume –Rehema na Amani zimshukie
–anaumathihsha uislamu na mfano wa jengo
kubwa, imara na madhubuti lililojengwa juu ya
nguzo tano. Hapana hata mmoja awezaye kupinga
kwamba kuna jengo linaloweza kusimama bila ya
nguzo. Kama tunakiri ukweli huu, basi ni dhahiri
kwamba hapana uislam pasipo na nguzo tano hizi
na pasipo na nguzo na uislam pana kufru tu si
vinginevyo. Eeh Mola wetu tukinge na ukafiri kwa
kutujulia kuisimamisha swala maisha yetu yote
Aamiyn. Inakupasa uelewe ewe nduguyangu mpenzi
muislam kwamba swala ndio nguzo tukufu kabisa ya
dini na nafasi na umuhimu wa swala katika
uislamu ni kama vile ilivyo nafasi na umuhimu wa
kichwa katika kiwiliwili. Basi kama ambavyo
asivyokuwa na uhai mtu asiye na kichwandivyo
ambavyo hana uislamumtu asiye na swala. Bwana
Mtume –Rehema na Amani zimshukie anatuasa kwa
kutuambia : "Ye yote atakuyeicha swala kwa
makusudi, bila ya shaka amekufuru"
Twabraaniy.
Haya hebu jiulize ewe Ndugu yangu Muislamu na
uihurumie nafsi yako, mtu aliyekufuru ana
Uislamu ?! Fahamu ewe Ndugu yangu unayemuasi
Mola wako kwa kuacha kuswali kwamba sala ndio
nguzo ya dini hii, dini haipo bila ya nguzo hii.
Haya yanathibitishwa na kauli ya Bwana Mtume –
Rehema na Amani zimshukie – "Swala ndio
nguzo ya dini, atakayeisimamisha, hakika
ameisimamisha dini na atakayeiacha, bila ya
shaka huyo ameivunja dini". Kwa mantiki
hii, mtu atakayeihifadhi nguzo hii kwa kuswali
katika nyakati zake maalumu na akatimiza sharti
na nguzo zote hali kujinyenyekeza kwa Mola wake
na huku akiamini kuwa ni wajibu wake kuswali,
huyo ndiye atakayefaulu duniani na akhera.
Tunasoma ndani ya Qur-ani Tukufu : "KWA
YAKINI WAMEFAULU WAUMINI AMBAO WAO NI
WANYENYEKEVU KATIKA SWALA ZAO" Al-Muuminun
: 1-2. Kinyume chake yule atakayeipuuzia swala,
akaacha kuswali, huyo ndiye mtu muovu aliyepata
khasara duniani na akhera kwa sababu ya
kuikhalifu amri ya Mola Muumba wake. Kwa mujibu
wa kauli iliyotangulia ya Bwana Mtume, wewe
usiotaka kuliweka paji lako la uso ardhini
kumsujudia Mola wako umeichukua nyundo kubwa na
nzito unaivunja na kuibomoa dini ya Mwenyezi
Mungu Mtukufu. Dini ambayo amewatuma mitume wake
wote, tangu Nabii Adam mpaka Mtume wa mwisho
Muhammad – Rehema na Amani ziwashukie wote –
kuja kuisimamisha katika katika ardhi hii. Je,
mbomoa dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu si mgomvi
wa Allah, na hivi mtu anaweza kugombana na Allah
kisha akatazamia kupata salama ?! La hasha.
Ewe mpenzi ndugu yangu, elewa na ufahamu
kwamba swala ndiyo ibada ya kwanza kabisa
aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake.
Amesema Bwana Mtume – Rehema na Amani
zimshukie - : "Cha mwanzo
alichokifaradhisha Allah kwa umati wangu ni
swala tano, na cha mwanzo kinachorufaishwa
(kinachopanda mbinguni) katika amali (matendo)
yao ni swala tano, na cha mwanzo watakachoulizwa
katika amali zao ni swala tano …." Ndugu
yangu mpenzi usiotaka kumsujudia Mola wako
aliyekuumba, haikutoshi hadithi hii kuona ni
jinsi gani ibada ya swala ilivyopewa umuhimu wa
kwanza katika Uislamu ?! Amali zako zote njema
ni lazima zitanguliwe na swala tano ndipo
zikubaliwe, kinyume na hivyo amali hizo hazina
maana bali ni sawa sawa na mavumbi
yapeperushwayo. Ushahidi wa haya ni kauli ya
Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie –
"Cha mwanzo
atakachokaguliwa/atakachohesabiwa mja siku ya
kiyama ni swala, ikitengenea zimetengenea baki
ya amali zake nyingine, ikifisidika (swala)
zimefisidika (zimeharibika) baki ya amali zake
nyingine"
Ndugu mpenzi muislamu, ukiyakiri maneno haya
ya Bwana Mtume yatakufikisha katika ukweli na
hakika kwamba swala ndio ibada mama. Kadhalika
ili kuonyesha utukufu wa ibada ya swala,
utaikuta swala ndio ibada pekee aliyoitiwa Bwana
Mtume na kukabidhiwa na Mola wake mbinguni.
Ibada nyingine zote Bwana Mtume alikuwa
akiletewa amri hapa hapa ardhini kupitia kwa
malaika Jibril – Amani imshukie – Allah
alimkuhutubu Mtume wake juu ya swala tano katika
ule usiku wa Miraji pasina wasita wa Jibril.
Amesema Anas – Allah amridhie –
Imefaradhishwa swala kwa Mtume – Rehema na
Amani zimshukie – usiku aliopelekwa mbinguni
swala khamsini, kisha zikapunguzwa mpaka zikawa
tano, kisha (Mtume) akaitwa ewe Muhammad !
Hakika maneno yangu hayabadilishwi na utapata
wewe katika swala tano hizo ujira wa swala
khamsini"
Ndugu yangu muislamu, hebu yatafakari kwa
makini maneno ya Mtume wako, utauona utukufu wa
ibada ya swala. Ni kwa ajili hiyo ndio tunaona
Allah anatuamrisha kuhifadhi na kudumisha swala
na muislamu amewajibikiwa kuitekeleza swala muda
wa kudumu roho yake katika kiwiliwili chake.
Akiwa mzima wa afya njema au mgonjwa asojiweza
kitandani kwa sharti ya kuwa na fahamu za kujua
alitendalo. Awapo vitani au katika hali ya
amani, akiwa safarini au la, swala imemlazimu
tu. Mwanamume na mwanamke wote ni sawa katika
amri hii ya swala, ila mwanamke hatoswali akiwa
katika hali ya hedhi au nifasi. Amesema Mwenyezi
Mungu Mtukufu katika kuamrisha swala
"HIFADHINI (angalieni sana) SWALA (zote
kuziswali) NA (khasa) ILE SWALA YA KATI NA KATI
NA SIMAMENI KWA UNYENYEKEVU KATIKA KUMUABUDU
ALLAH NA MKIWA KHOFU ( mmo vitani, basi swalini)
HALI YA KUWA MNAKWENDA KWA MIGUU AU MMEPANDA
(wanyama) NA MTAKAPOKUWA KATIKA AMANI BASI
MKUMBUKENI ALLAH (swalini) KAMA ALIVYOKUFUNZENI
YALE MLIYOKUWA HAMYAJUI" [2:238-239]
Ndugu yangu mpenzi, utabainikiwa kutokana na
aya hii kwamba muislamu hana udhuru hata chembe
unaomuhalalishia kuacha swala. Hivyo basi
muislamu atakayeitekeleza swala kama
itakikanavyo, swala hiyo itakuwa ni hoja (wakili
wa kumtetea) itakayomuokoa siku ya Kiyama, si
hivyo tu bali itakuwa ni nuru itakayomuangazia
na kumuongoza katika siku hiyo ngumu na nzito
kama ambavyo itakovyokuwa ni sababu ya kufutiwa
madhambi yake. Imepokelewa kutoka kwa Sayyidna
Uthman – Allah amuwie Radhi – amesema :
nimemsikia Mtume – Rehema na Amani zimshukie
– akisema : "Hatawadhi mtu udhu wake
vizuri kisha akaswali ila Allah humsamehe mtu
huyo madhambi yaliyo baina ya swala hii na swala
ijayo". Basi ni kheri na furaha iliyoje kwa
yule aliyeitekeleza swala kwa ukamilifu,
ukamilifu na unyenyekevu mpaka anamaliza muda
wake wa kuishi hapa duniani (anakufa). Eh! Ole
wake, tena ole wake na majuto yake yule
aliyefanya kibri, akaacha kuitekeleza swala hata
akaondoka duniani bila ya kumsujudia Mola wake.
Hebu itegee sikio la usikivu kauli hii tukufu ya
Allah asema nini juu ya watu hawa : "(Na
wawalete) HIYO SIKU KUTAKAYOKUWA NA MATESO
MAKALI NA WATAITWA KUSUJUDU LAKINI HAWATAWEZA.
MACHO YAO YATAINAMIA CHINI; UNYONGE UTAWAFUNIKA
NA HAKIKA WALIKUWA WAKIITWA KUSUJUDU WALIPOKUWA
SALAMA (na walikataa)" [68:42-43].
Watu wa peponi watawauliza watu wa motoni :
"NI KIPI KILICHOKUPELEKENI MOTONI ? WASEME
: HATUKUWA MIONGONI MWA WALIOKUWA WAKISWALI.
HATUKUWA TUKILISHA MASIKINI. NA TULIKUWA
TUKIZAMA (katika maasia) PAMOJA NA WALIOKUWA
WAKIZAMA" [74:42-45]. Khasara na maangamivu
yaliyoje, leo utawaona baadhi ya waislamu
hawaswali na hoja yao kubwa shughuli nyingi
hawana nafasi, wametingwa na kazi na wengine
huthubutu hata kusema kwa kinywa kipana kabisa
kwani ni lazima kuswali, kama ninafanya mema
mengine haitoshi ?! Hebu itegee sikio kauli hii
ya Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie - :
"Yeyote yule atakayeihifadhi swala, iatkuwa
(swala hiyo) ni nuru, hoja na uokovu kwa mtu
huyo siku ya Kiyama, na yeyote yule
asiyeihifadhi swala, haitokuwa (swala) ni nuru,
hoja na uokovu kwa mtu huyo, bali atakuwa
(motoni) siku ya Kiyama pamoja na akina Qaarun,
Fir-aun, Haaman na Ubayyi bin Khalaf".
Fahamu ewe ndugu yangu muislamu, swala ina
nafasi na utukufu wa pekee katika Uislamu ndio
maana tunamkuta Bwana Mtume mara nyingi
anatuhimiza swala na swala ndio ulikuwa wasia
wake wa mwisho wakati anaondoka duniani :
"Ninakuhimizeni na kukuusieni swala pamoja
na wamilikiwa wa mikono yenu ya kuume".
C. KHATARI YA KUACHA SWALA
Ndugu yangu Muislamu, bila shaka unatambua au
umewahi kusikia kwamba Allah aliwaamrisha
malaika pamoja na Ibliis wamsujudie baba yetu
Nabii Adam – Amani imshukie – hali ya
kumuamkia. Iblisi kwa ushupavu na kibri
alichokuwa nacho alikataa kuitii na kuitekeleza
amri ya Mola wake. Ni kwa sababu hii tu Allah
akamfukuza Iblis na kumtoa huko alikokuwa pamoja
na Malaika na akamlaani mpaka siku ya kiyama, na
kesho akhera ataingia motoni. Tusome kwa
mazingatio : "(na wakumbushe watu khabari
hii) TULIPOWAAMBIA MALAIKA MSUJUDIENI ADAM (
yaani mwadhimisheni kwa ile elimu yake
aliyopewa) WAKAMSUJUDIA WOTE ISIPOKUWA IBLIS,
AKAKATAA NA AKAJIVUNA NA (toke hapo) ALIKUWA
KATIKA MAKAFIRI (ila tu alichanganyika tu na
malaika)" [2:34].
Basi wewe ndugu yangu mpenzi usiotaka
kuswali, hujioni kuwa wewe ni mbaya zaidi kuliko
Iblis ?! Iblis alikataa kumsujudia Nabii Adam,
wewe leo unakataa kumsujudia aliyemuumba Nabii
Adam. Iblis alikataa kusujudu mara moja tu, wewe
leo unakataa kusujudu mara thelathini na nne
(34) kila siku, mara 238 kila wiki, mara 1020
kila mwezi, mara 12,104 kwa mwaka, mara …..
katika umri wako, jaza mwenyewe. Iblis alikataa
kusujudu sijida ya heshima kwa Nabii Adam, wewe
unakataa kusujudu sijida ya ibada kwa Mola
Muumba wako. Hebu angalia tena adhabu aliyopewa
Iblis kwa kuacha sijida moja tu alilaaniwa na
kutolewa peponi na huku akisubiriwa kuliongoza
kundi la watu wa motoni kuingia motoni. Hii
inamaanisha mwenye kuacha sijida 34 kila siku
anastahiki kupata adhabu kali zaidi ya ile
aliyopewa Iblis mlaaniwa, sikwambii asioswali
juma moja au zaidi. Ndugu yangu usioswali
unatarajia nini ikiwa hali ni hiyo ?! Unaona
uzito gani kumsujudia Mola wako ?! Aletwe Mtume
mwingine ndio utasikia na kutii ?! Hebu ihurumie
nafsi yako, huiwezi adhabu ya Mola wako. Ndugu
yangu umepewa neema ya akili, ishukuru neema
hiyo kwa kuzingatia uambiwayo, umepewa masikio
ili usikie, isikie haki na kuifuata, usijitie
upofu na uziwi wa bure ukajuta na kuangamia.
Zinduka, usiingie katika kauli ya Allah isemayo
: "NA BILA SHAKA TUMEWAUMBIA MOTO WA
JAHANAMU WENGI KATIKA MAJINI NA WANADAMU (kwa
sababu hii): NYOYO WANAZO LAKINI HAWAFAHAMU
KWAZO, NA MACHI WANAYO LAKINI HAWAONI KWAYO, NA
MASIKIO WANAYO LAKINI HAWASIKII KWAYO. HAO NI
KAMA WANYAMA, BALI WAO NI WAPOTOFU ZAIDI. HAO
NDIO WALIOGHAFILIKA" [7:179].
Tahadhari ewe ndugu yangu, usiwe na sifa hizi
zilizotajwa, kwani hizi ni sifa za watu wabaya,
watu wa motoni. Tumuombe Mola wetu Mtukufu
asitujaalie kuwa miongoni mwa watu wa motoni,
wasiotaka kumsujudia – Amin.
|