|
NDOA
NA RIZIKI NJEMA...VI
Ndoa
kama msingi mkuu wa familia si jambo jepesi ambalo huwa kwa, makubaliano
na maridhiano baiana ya pande mbili, mwanamume na mwanamke ambao huamua
kuchanganyika pamoja na kuanza maisha kama mtu na hawara yake. Hizi ni
fikra potofu dhidi ya suala hili zito la ndoa, ni wajibu zisahihishwe.
Ndoa ni suala lenye umuhimu wa pekee na nafasi kubwa katika Uislamu. Hili
linatokana na kuwa kwake ndio msingi wa familia ambazo ndizo zinazounda
jamii ya wanadamu. Ni kutokana na uzito wake huu ndio tunamkuta Mwenyezi
Mungu Mtukufu analihusisha suala la ndoa na riziki njema, akasema, NA
ALLAH AMEKUUMBENI WAKE KATIKA JINSI YENU, NA AKAKUJALIENI KUTOKA KWA WAKE
ZENU WATOTO NA WAJUKUU NA AKAKURUZUKUNI
VITU VIZURI VIZURI…………” (16:72)
Angalia
jinsi Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyotuwekea utaratibu na mpango mzuri wa
maisha yetu. Mpango huu si mwingine zaidi ya ndoa. Kupitia ndoa
anaturuzuku bila ya maombi yoyote kutoka kwetu watoto, wajukuuu sambamba
na riziki njema. Haya ni baadhi ya matunda peni ya utaratibu huu wa Allah
kwetu sisi waja wake. Hakuna hata mmoja asiyeufahamu umuhimu wa watoto kwa
wazazi, asiyejua umuhimu huu amuangalie mtu ambaye hajajaliwa kupata mtoto
namna anavyohangaika huku na kule. Suala la riziki na umuhimu wake katika
maisha yetu ya kila siku halina kificho kwa kila mmoja wetu. Ikiwa
Mwenyezi Mungu Mtukufu anaithamini riziki njema kupitia ndoa, kipi basi
kianchofanya uzini na ukaacha kuoa? Je, huiamini ahadi ya Mola wako, Mtoa
riziki? NA WAOZENI WAJANE MIONGONI MWENU (waungwana) NA WALIO WEMA KATIKA
WATUMWA WENU(wanaume) NA WAJAKAZI WENU, KAMA WATAKUWA MAFAKIRI ALLAH
ATAWATAJIRISHA KATIKA FADHILA ZAKE, NA ALLAH NI MWENYE WASAA, MWENYE KUJUA:
(24:32).
UIMARISHAUJI
WA MAFUNGAMANO BAINA YA MUME NA MKE……VII
Uhusiano
mwema masikilizano na maelewano ndani ya nyumba ni miongoni mwa mambo
ambayo yanaimarisha mafungamano haya ya ndoa baina ya mume na mke. Kuwepo
kwa mafungamano imara baina ya wawili hawa kupelekea kuzidi kwa mapenzi,
huruma na utulivu. Nyumba iliyosheheni mapenzi, huruma na utulivu, huwa ni
pumbazo la nafsi na raha yenye furaha kwa kila mmoja, mume na mke. Hili
ndilo analolisema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake NA KATIKA
ISHARA ZAKE (za kuonyesha ihsani zake juu yenu) NI KUWA AMEKUUMBIENI WAKE
ZENU KATIKA JINSI YENU ILI MUPATE UTULIVU KWAO, NAYE AMEJAALIA MAPENZI NA
HURUMA BAINA YENU……..” (30:21) Mwanadamu hawezi kuifurahia neema ya
watoto wala hawai pambo a masiha yake kama nyumba yake haikutawaliwa na
utulivu na akaishi chini ya
anaga la mapenzi na huruma na hapo ndipo mke na watoto huwa ni burudani ya
macho aliyoileza Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake tukufu. (NA WALE
WANAOSEMA: “ MOLA WETU! TUPE KATIKA WAKE ZETU NA WATOTO WETU
YABURUDISHAYO MACHO( yetu) nyoyoi zetu) NA UTUJAALIE KUWA WAONGOZI KWA
WAMCHAO (Allah) “ (25:74)
Ni
kutokana na umuhimu huu wa suala la ndoa kwa mwanadamu ndio maana Uislamu
ukaishughulikia sana ndoa. Uislamu ukaiwekea ndoa sheria na kanuni
madhubuti zenye dhima ya kuhakikisha inafikia kilele cha malengo yake.
Sheria na kanuni hizi zinamjengea mwanadamu mazingira bora, mazingira
tayarifu ya ndoa. Miongoni mwa aya za Qur-ani Tukufu na hadhithi za Mtume
zinatoa maelekezo juu ya ndoa ni hizi zifuatazo:
i)
Uchaguzi wa mke/mume
Tunasoma
kuhusiana na suala zima la uchaguzi wa mke:”……BASI WANAWAKE WEMA NI
WALE WENYE (waume zao) KWA KUWA ALLAH AMEWAAMRISHA WAJIHIFADHI……”
(4:34)
Bwana
Mtume – Rehema na Amani zimshukie – anatupa vigezo vya kuolewa
mwanamke kupitia riwaya iliyopokelewa na Abu Hurayrah Allah amuwiye radhi
– kutoka kwa Mtume amesema:
Mwanamke
huolewa kwa mambo manne:
-
Kwa
mali yake
-
Na
uzuri wake
-
Na
nasabu zake
-
Na
dini yake.
Basi
mchague mwenye dini itabariki
mikono yako” Jaamiy swaghiyr. Ili kujenga familia bora Uislamu
haukomelei tu kumpa mwanamume vigezo vya kuchagua mke mwema na kumsahau
mwanamke kwa kuzingatia kuwa ni mwanamke na mwanamume pamoja ndio
wanaounda ndoa, Uislamu umemuelekeza mwanamke pia amchague nani kuwa mume
mwandani na mshiriki mwenza katika maisha. Kigezo pekee ni dini na tabia
kama alivyoeleza Bwana Mtume-Rehema na Amani Zimshukie.
ii)
Ahadi Thabit
Uislamu
kwa kuizingatia dhima na umuhimu wa ndoa katika maisha ya mtu binafsi
familia na jamii umeifanya ndoa kuwa ni mkataba. Mkataba huu unahusisha
mambo yafuatayo kama nguzo.
1.
Matamko ya “Iijaab” na Qabuul”
Ø
“Ijabu” hili ni tamko
linalotoka wa walii wa mwanamke kumwambia muaoji (mume mtarajiwa) wakati
wa kufunga mkataba huu. Tamko hili ni kusema “NIMEKUUOZA “ Fulani.
Ø
“Qabuul” hili ni tamko analolitamka muoaji kumwambia walii.
Husema “NIMEKUBALI KUMUOA” Fulani
2.
Mashahidi.
Hawa
ni watu watakaoshuhudia mkataba wa ndoa ukifungwa.
3.
Walii wa mke.
Huyu
ni mtu mwenye mamlaka ya kumuozesha mwanamke. Huyu ndiye anayeusimamia
mkataba huu kwa niaba ya mwanamke, kwa sababu katika Uislamu mwanamke
hajiozeshi yeye mwenyewe. Mtu huyu huwa ni baba mzazi, baba mzaa baba,
kaka wa tumbo moja, mwanawe kaka, ami (baba mdogo/mkubwa) na kuendelea
kama walivyobainishwa katika vitabu vya fiq-hi.
4.
Bwana na Bibi harusi (mume na mke)
Hawa
ndio wanopeana ahadi thabiti ya kuishi kama mume na mke chini ya muongozo
na maelekezo ya Mola jwao. Hupeana ahadi ya kushirikiana katika matamu na
machungu ya maisha. Hupeana ahadi ya uaminifu na ukweli ya kwamba kila
mmoja wao atachunga heshima ya mwenziwe, hataisaliti ndoa yao. Ahadi hii
wanayopeana katika mkataba huu haina budi kulindwa na kuheshimiwa na kila
mmoja wao. Kwa sababu ndio inayowaunganisha pamoja kimwili, kiroho na
kijinsia ikawafanya wakazoeana kwa muda mfupi tu kuliko hata ndugu
waliozaliwa na baba na mama mmoja. Hii ndio ahadi thabiti ndani ya kitabu
chako kitukufu. “NA KAMA MKITAKA KUBADILISHA MKE MAHALI PA MKE (yaani
kumuoa mke mwingine na kumuacha huyo wa zamani) NA HALI MMOJA WAO (naye
ndiye huyo unayemuacha) MMEMPA MRUNDI WA MALI, BASI MSICHUKUE CHOCHOTE (msimnyang’nye).
JE, MNACHUKUA KWA DHULMA NA HATIA ILIYO WAZI? NA MTACHUKUAJE NAHALI NYINYI
KWA NYINYI MMEINGILIANA? NAO (wanawake) WAMEPOKEA KWENU AHADI THABITI (kuwa
mtakaa nao kwa uzuri)” (4: 20-21)
Katika
kuutekeleza mkataba huu wa ndoa na kumtekelezea mke haki yake, Mwenyezi
Mungu Mtukufu anatuambia: ‘ NAO (wanawake) WANAYO HAKI KWA SHARIA (kufanyiwa
na waume zao) KAMA ILE HAKI ILIYO JUU YAO KUWAFANYIA WAUME ZAO….”
(2:228)
KUZAANA
NI MAENDELEO YAKIMAUMBILE YA KIZAZI CHA WANADAMU…….VIII
Mwenyezi
Mungu Mtukufu amemleta mwanadamu katika maisha haya kwa lengo maalum. Ili
aweze kulitekeleza lengo hili akamuandalia na kumuwekea utaratibu maalum
utakaomletea kaika uhai huu, mahala pa kulitekelezea lengo la uumbwaji
wake. Kwa upande mwingine mwanadamu ameumbwa katika maumbile ya kupenda
kuishi milele bila ya kufa. Lakini hili ni jambo asilolimiliki, kwa hiyo
njia pekee ya kuishi milele na kuendelea kukumbukwa ni kupitia kuzaana
katika ndoa. Akipata watoto ataitwa baba/mama , babu/bibi hata baada ya
kufa kwake bado familia yake itaendelea kujifakharisha na kujiita kwa jina
lake (kujinasibisha nae). Kwa hivyo basi ndoa inakuwa ni sababu aliyoiweka
Allah ya kuendeleza kizazi cha wanadamu, tusome, NA ALLAH AMEKUUMBIENI
WAKE KATIKA JINSI YENU NA AKAKUJAALIENI KUTOKA KWA WAKE ZENU WATOTO NA
WAJUKUU NA AKAKURUZUKUNI VITU VIZURI VIZURI…….” (16:72)
|