|
Ukimwi ni maradhi hatari sana yaliyogubika ulimwengu mzima. Maradhi
haya nitisho kubwa sana kwa maisha ya binaadamu kwa sababu mpaka sasa mabingwa wa sayansi
ya tiba hawajagundua kinga wala tiba yake. Inakadiriwa kuwa takribani watu milioni 13
wamekwishaambukizwa virusi vya gonjwa hili hatari ulimwenguni kote. UKIMWI kwa kishwahili,
AIDS kwa kiingereza herufi za neno UKIMWI ndizo zinazobeba na kuwakilisha jina la ugonjwa
hu harati, U = Ukosefu, KI wa kinga. MWI mwilini. Mwenyezi Mungu Mtukufu
ameuzawadia mwili wa binadamu jeshi miongoni mwa majeshi yake mengi
"
.WALA HAPANA YOYOTE AJUAYE MAJESHI YA MOLA WAKO ILA YEYE
TU
.. 74:31
Majeshi hayo yaliyojikusanya pamoja ambayo hayaonekani kwa jicho tupu
ila kwa msaada wa darubuni maalumu hupambana na kukishambulia kila
kirusi/bacteria/kijidudu chochote cha maradhi kinachojipenyeza ndani ya mwili wa binadamu.
Majeshi haya yakizidiwa na kushindwa ndipo kirusi/bacteria huushambulia mwili na
kusababisha maradhi mwilini. Maradhi haya hatari ya ukimwi yanapouvaa mwili ndio
huyasagilia mbali majeshi haya yaliyowekwa mwilini kwa nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu,
hapo ndipo mwanadamu huweza kushambuliwa kwa urahisi uhai wake. Haya ndio maradhi
yajulikanayo kwa jina la UKIMWI (AIDS), maradhi ambayo yanautikisa ulimwengu mzima hivi
sasa na kuwafanya wana sayansi kukesha katika maabara zao ikiwa ni katika jitihada za
kujaribu angalau kugundua tiba au kinga yake ili kuikoa jamii ya wanadamu kutokana na
janga hili la kutisha. Ulimwengu mzima unapiga kelele, wanasiasa, viongozi wa kidini
misikitini na makanisani wote wanafanya juhudi za kuelimisha na kuitahadharisha jamii juu
ya maradhi haya. Mapesa chungu nzima yametolewa na serikali na mashirika mblaimbali katika
kuelimisha na kuupiga vita ugonjwa huu, vitabu vimetungwa na filamu zimeandaliwa sambamba
na mabango. Hebu tujiulize ni nini hasa sababu ya yote haya? Ni kitu/jambo gani
lililotumbukiza ulimwengu katika janga hili? Nani hasa wa kulaumiwa kutokana na janga
hili?
Naam, ni ukweli usiopingika na ni hakika iliyo wazi dhahiri kwa kila
mmoja wetu kuwa UKIMWI ni matokeo ya binadamu kulibadilisha umbile la Mwenyezi Mungu
alilowaumbia watu, ni natija ya kubadilisha na kukengeusha kanuni za maumbile ya ulimwengu
huu, ni sababu ya kuzipa mgongo hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu.
Tusome kwa mazingatio BASI UELEKEZE USO WAKO KATIKA DINI ILIYO
SAWASAWA, NDILO UMBILE ALALH ALILOWAUMBIA WATU(Yaani dini hii ya kiislamu inawafikiana
barabara na umbo la binadamu ) HAKUNA MABADILIKO KATIKA MAUMBILE YA VIUMBE VYA ALLAH. HIYO
NDIYO DINI ILIYO HAKI, LAKINI WATU WENGI HAWAJUI" (3:30). Ukaidi wa binadamu kuipinga
haki na kutokuifuata ndio ulioifikisha hapa tulipo leo, nguvu kazi (vijana ) ya jamii,
muhimili (wazee) wa jamii na rasilimali ya jamii inapotea na kumezwa na janga hili la
ukimwi.
Mpaka malaika (watoto wadogo) walionao matumboni mwa mama zao tayari
wamshaambukizwa na kuathirika na maradhi haya mabaya. Ni nani anayedhulumu uhai wao
malaika hawa, kwani ni dhahiri kuwa hawatakuwa na muda mrefu wa kuyafurahia maisha haya,
kabla kifo hakijawarejesha kwa Mola wao. Bila shaka dhalimu hapa ni mwenye kukhalifu
sheria ya Mwenyezi Mungu. Maradhi haya ndiyo jazaa ya uoni na uchafu anaoufanya mwanadamu,
ni malipo ya kuenea na kutapakaa kwa dhambi ya zinaa na liwati, ni thawabu za kuingiliana
kimwili wanamume kwa wanamume, ni zawadi ya klabu za usiku (makasino) ni tuzo ya uhuru wa
kuchanganyika mwanaume na wanawake katika msingi ya kile kinachoitwa usawa. Hayo ndio
matokeo ya maendeleo tunayoyaiga kutoka kwa watu walioendelea wa Magharibi watu waliofika
mwezini na sasa wanajaribu kwenda katika sayansi nyingine. Hawa ndio watu huru, wasemao
tuacheni tufanye tutakavyo maadamu hatuvunji sheria za nchi, tuoane wanamume kwa wanamume
na wanawake kwa wanawake. Serikali zao zikawakubalia na mabunge yao ya kapitisha sheria
wakawa na wawakilishi bungeni, na wanamume wakaoana kisheria na hati za ndoa kutolewa na
ndoa hiyo kushuhudiwa pengine hata na viongozi wa kiserikali na picha zikapigwa uchafu huu
na fisadi hii ndio iliyoufikisha na kuutumbukiza ulimwengu katika janga hili la maradhi
mabaya ya ukimwi. Tusome na tuyafanyie kazi "UHARIBIFU UMEDHIHIRI BARANI NA BAHARINI
KWA SABABU YA YALE ILIYOYAFANYA MIKONO YA WATU (maovu) ILI AWAONJESHE (adhabu ya) BAADHI
YA MAMBO WALIYOYAFANYA, HUENDA WAKARUDI (wakatubia kwa Mola wao) (30:41). tuzidi
kuwaidhika: NA MISIBA (majanga) INAYOKUPATENI NI KWA SABABU YA VITENDO VYA MIKONO
YENU (Maoni)
. (42:30). Tafsiri potofu ya uhuru itolewayo na Magharibi ndio
kiini cha janga hili. Uhuru na ufuska si uhuru wa haki, uhuru wa kinyama si uhuru wa haki,
uhuru hakika si mtu kufanya apendavyo na kutamani lakini uhuru wa kweli ni mtu kufanya
atakiwayo kufanya (yaliyompasa). Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka katika ulimwengu huu,
kila kitu kina mpaka wake maswahaba walimuuliza Bwana Mtume- Rehema na Amani zimshukie-
kuhusiana na mtu kukutana na mkewe katika kipindi cha hedhi, ikashuka kauli ya Mwenyezi
Mungu Mtukufu kuwajibu "NA WANAKUULIZA JUU YA HEDHI; WAAMBIE HUO NI UCHAFU: BASI
JITENGENI NA WANAWAKE WAKATI WA HEDHI (zao) WALA MSIWAKARIBIE MPAKA WATWAHARIKE.
WAKISHAKUTWAHARIKA BASI WAENDEENI KATIKA PALE ALIPOKUAMRISHENI ALLAH. HAKIKA ALLAH
HUWAPENDA WANAOTUBIA NA HUWAPENDA WANAOJIITA KASA. (2:222)
Aya inahalalisha kuwaingilia wanawake, na sio kuwaingilia popote bali
mahali pa shamba (patoapo mazao) tena muingiliano huo uwe ni kati ya mtu na mkewe wa
halali. Lakini utakapofika wakati wa adha (hedhi) basi imempasa mume kujizuia na
kuidhibiti nafsi yake mpaka mkewe atwaharike kwa kumalizika hedhi yake. Ama mtu kutenda
kinyume cha hivi, akapaendea mahala pengine, mahala pa uchafu ambapo hapakuumbwa kwa ajili
ya tendo hili la ndoa, mahala pasipootesha mimea huko ni kuyabadilisha maumbile ya
Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanamume kuwa ni mfanywaji apandwe bali awe ni
mfanyaji apande yeye wala hakuiumba duburi (utupu wa nyuma) kwa ajili ya kuingiliwa bali
kwa kazi maalumu na muhimu. Kazi hii si nyingine ila kutoa nje makapi ya chakula
yasiyohitajika mwilini ambayo kama hayakutoka binadamu hawezi kuwa binadamu mwenye afya na
siha njema. Kila kiungo katika mwili wa binadamu kimeumbwa kwa lengo/kazi maalumu ambayo
haiwezi kufanywa na kiungo, kingine ila hicho hicho tu, sasa kukitumia kiungo kwa kazi
isiyo yake, huko si kubadilisha umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia waja wake? Ni ufundi
huu wa binadamu kijifanya mjuzi kuliko Muumba wake na kubadilisha kanuni za maumbile ndio
uliotufikisha kuogelea, katika bahari hii ya ukimwi. Kwa mtaji huu hatujui ni nini
kitafuatia baada ya ukimwi! Historia inatuonyesha kuwa watu waliufanya ufundi huu wa
kubadilisha umbile la mwenyezi Mungu nao si wengine bali ni kaumu ya Nabii Lutwi hawa ndio
viumbe na kwanza kuanzisha uovu na uchafu huu wa kuingiliana wanamume kwa wanamume. Tusome
na tuzingatie. NA (tulimpeleka) LUTWI. BASI (wakumbushe watu wako) ALIPOWAAMBIA
KAUMU YAKE JE! MNAFANYA JAMBO CHAFU AMBALO HAJAKUTANGULIENI YOYOTE KWA (jambo chafu) HILO
KATIKA WALIMWENGU!.(7:80)
Mwenyezi Mungu aliwapelekea waja wake hawa mtume wake Lutwi Amani
imshukie awaite kwake na wauache uchafu huu Akawaambia (Lutwi): MNAWAINGILIA
WANAMUME KWA MATAMANIO MABAYA BADALA YA WANAWAKE? HAKIKA NYINYI NI WATU MFANYAO YA UJINGA
KABISA (27:55) Akawaambia tena: NYINYI MNAWAENDEA WANAMUME KWA KUWA NDIO
MNAOWATAMANI BADALA YA WANAWAKE! AMA NYINYI NI WATU WAFUJAJI. (7:81) Akazidi
kuwaasa, NA MNAWACHA ALICHOKUUMBIENI MOLA WENU KATIKA WAKE ZENU? KWELI NYINYI NI
WATU MNAORUKA MIPAKA (mliyowekewa) (26:166)
. BILA SHAKA WAO WALIKUWA WATU WABAYA, WAVUNJAO
AMRI. (21:74) Nabii Lutwi aliwasifia watu hawa kwa kila sifa mbaya kutoka na kitendo
chao hiki kichafu, kisha akamuomba Mola wake amuepushe na watu waovu hawa walioitia doa
historia nzima ya jamii ya wanadamu. Nae Mwenyezi Mungu akalikubali ombi la Mtume wake na
akamuokoa na watu wa ule mji uliokuwa ukifanya maovu. Hakika hili ni janga na msiba,
atakayesibiwa na msiba huu, akili humtoka, utu humvuka na mahala pake kukaliwa na unyama
kwa maana ya unyama. Hawa walistahiki kufikwa na adhabu ya Mola wao na waliadhibiwa kwa
adhabu ambayo Mwenyezi Mungu hajapata kuadhibu kwa adhabu kama hiyo kwa kaumu
zilizowatangulia na zilizokuja baada yao ikiwa ni jazaa ya uovu na uchafu wao ambao
haukupatwa kufanywa na ye yote kabla yao. Tusome, tuwaidhike na tuonyeke BASI
ILIPOFIKA AMRI YETU, TULIIFANYA (ardhi hiyo iwe juu chini) JUU YAKE KUWA CHINI YAKE NA
TUKAWATEREMSHIA MVUA YA CHANGARAWE ZA UDONGO MGUMU (wa motoni uliokamatana) (changarawe)
ZILIZOTIWA ALAMA KWA MOLA WAKO (kila moja kuwa ya mtu fulani)NA (adhabu) HII HAIKO MBALI
NA MADHALIMU (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya). (11: 82
83)
Leo baadhi yetu wamerudia kuufanya uchafu huu ulioasisiwa na kaumu ya
Mutme Lutwi, wakauonea fakhari na kuutangaza dhahiri bila kificho mpaka kufikia hatua ya
kuuhalalisha kwa kuoana na kuwa na klabu zao maalumu na kujitangaza katika vyombo vya
habari. Kiovu zaidi walichowashinda hawa wa leo wale wa zamani wa kaumu Lutwi ni kwamba
hawa wa leo wana kanuni/sheria zinazowalinda na kuwahalalishia biashara yao hii chafu
zilizotungwa na mabunge ya nchi zao na serikali zao kuwatoza kodi kwa mapato machafu
wanayoyapata kutokana na biahara yao hii chafu. Kwa masikitiko makubwa yapo baadhi ya
makanisa katika nchi fulani fulani yanathubutu kulibariki tendo hili chafu makanisa
yanayojinasibisha na Nabii Isa mwana wa Mariam Amani imshuku ambaye alikuwa akisema
"waliokuwa kabla yenu walikuwa wakisema usizini na mimi ninasema Atakayetazama kwa
macho yake, atakuwa amezini". Hivyo ndivyo tunavyosoma katika Injili. Nabii Issa
anaharamisha kutazama, vipi basi, viongozi hawa wa kamanisa wanajasiri kuhalalisha
aliyoyaharamisha Mungu kupitia kwa Mitume wake wote akiwemo Nabii Issa ambao wao wanadai
kumfuata?! Wanaupa baraka zote uchafu na uoza huu Ni ustaarabu gani huu?! Tunaelekea
wapi?! Turudi ndugu zanguni, UKIMWI hauna dawa, tutakwisha, Kondomu sio kinga ya ukimwi,
kinga na dawa pekee dhidi ya maradhi haya ya hatari ni kurejea kwa Mola wetu,
tujisalimishe kwake kwa kufuata hukumu na sheria zake. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuhifadhi
na kutukinga kwa mafundisho ya dini yake na hukumu za sheria yake na itikadi ambayo
humfanya muumini kuwa imara kama jabali madhubuti mbele ya matamanio machafu na maovu
kiasi cha kutokutetereka. Uislamu umemlea mwanadamu kuinamisha macho na kuhifadhi utupu
wake, tusome na tunaisihike: WAAMBIE WAISLAMU WANAUME WAINAMISHE MACHO YAO (wasitazame
yaliyokatazwa) NA WAZILINDE TUPU ZAO, HILI NI TAKASO KWAO, BILA SHAKA ALLAH ANAZO HABARI
ZA (yote) WANAYOYAFANYA. NA WAAMBIE WAISLAMU WANAWAKE WAINAMISHE YAO NA WAZILINDE TUPU
ZAO, WALA WASIDHIHIRISHE VIUNGO VYAO ISIPOKUWA VINAVYODHIRIKA (nao ni uso na vitanga) NA
WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO NA WASIONYESHE MAPAMBO YAO
. (24: 30
31)
Uislamu umemlea muumini katika malezi ya kutochanganyika kimwili ila
katika halali (ndoa) Mongoni mwa sifa walizosifiwa nazo waumini ndani ya Qur-ani ni:
NA AMBAO TUPU ZAO WANAZILINDA ISIPOKUWA KWA WAKE ZAO TU AU KWA (wanawake) WALE
ILIYOWAMILIKI MIKONO YAO YA KUUME. BASI HAO NDIO WASIOLAUMIWA. (Lakini) ANAYETAKA KINYUME
CHA HAYA, BASI HAO NDIO WARUKAO MIPAKA (ya Allah) (23: 5 7)
Uislamu umemfungia muislamu milango na mianya yote ya haramu sambamba
na kumfungulia milango ya halali
BASI OENI MNAOWAPEMDA KATIKA WANAWAKE
(maadamu mtakuwa waadilifu) WAWILI, AU WATATU AU WANNE (tu) NA MKIOGOPA KUWA HAMUWEZI
KUFANYA UADILIFU, BASI (oeni) MMOJA TU
(4 : 3)
Sasa wanadamu wanapoyatupilia mbali mafundisho haya ya Mola wao na
kufuata matashi na matamanio ya nafsi zao kwa kutneda yale ya haramu yenye kubadilisha
umbile lao waliloumbiwa, hao wamestahiki kupata adhabu kali ya Mwenyezi Mungu aliye mkali
wa kuadhibu. Mbali na zile adabu/adhabu za kisheria alizompa mamlaka kiongozi aongozaye
kwa kutumia Qur-ani kuzitekeleza kama vile kumkata mkono mwizi, kumcharaza bakora mzinifu
au kumpiga mawe mpaka afe na nyinginezo pia ana adhabu za kimaumbile zinazotawaliwa na
nguvu yake ya utendaji. Maradhi haya ya ukimwi yanaingia katika kundi hili la adhabu za
kimaumbile kama alivyotutanabalisha na hilo Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie katika
hadithi iliyopokelewa na Ibn Maajah, Al-Haakim na Al-Bayhaqiy ikiwa ni upokezi wa Ibn Umar
Allah awawie radhi kwamba Mtume aliwaambia maswahaba wake. Enyi kusanyiko la
Muhajirina, mtakapotahiniwa kwa mambo matano na ninajilinda kwa Mwenyezi Mungu msiyadiriki
(na likawa la mwanzo la matano hayo) haukudhihiri uchafu (zinaa) katika kaumu katu
(kabisa) mpaka wakautangaza wazi wazi ila itaenea kwao tauni na magonjwa ambayo hayakuwepo
kwa wahenga wao walipita
Naam, ni kweli ukimwi nido tauni ya zama hizi na ni kweli kuwa
maradhi haya mabaya hayakuwepo huko nyuma bali yamezuka hivi karibuni tu, ni kweli kabisa
haya ni maradhi mapya. Watu wamezua uchafu na uovu na Mola wao amewazushia adhabu. Enyi
mliopotea rudini, enyi waasi tubieni, Mwenyezi Mungu anajtuambia NA MISIBA
INAYOKUPATENI NI KWA SABABU YA VITENDO VYA MIKONO YENU, NA (juu ya hivi Allah) ANASAMEHE
MENGI. (42:30).
.. ILI AWAONJESHE (adhabu ya) BAADHI YA MAMBO
WALIYOYAFANYA HUENDA WAKARUDI (wakatubia kwa Allah). (42:41)
Yaani Mwenyezi Mungu anawazindua waja wake kwa adhabu za maradhi kama
haya ya ukimwi ili warejee kwake. Basi,
je, watarejea waliokengeuka?!
Je, watatubia waasi hawa?!
Je, wataongoka wapotevu hawa?!
Je, wataongoka wapotevu hawa?!
Je, watazinduka walioghafilika?!
Je watatubia waasi hawa?!
Je, wataongoka wapotevu hawa?!
Je, watazinduka walioghafilika?!
Je, wataamka wale wote waliolala?!
Tunasihike: "
BASI JE, MTAACHA (mabaya hayo). (5:91)
|