|
Muislamu hulichukulia suala la uvaaji kuwa ni miongoni mwa amri za Mola wake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu : "ENYI WANAADAMU! CHUKUENI MAPAMBO YENU (vaeni nguo
zenu nzuri) WAKATI WA KILA SWALA; NA KULENI (vizuri) NA KUNYWENI (vizuri). LAKINI MSIPITE
KIASI TU. HAKIKA YEYE (Allah) HAWAPENDI WAPITAO KIASI" [7:31]
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa ruhusa waislamu wale, wanywe na wavae vizuri na pia
waende msikitini wakiwa wamevaa nguo nzuri. Na amesema tena : "ENYI WANADAMU! HAKIKA
TUMETEREMSHIENI NGUO ZIFICHAZO TUPU ZENU NA NGUO ZA PAMBO; NA NGUO ZA UTAWA (ucha-mungu)
NDIZO BORA
" [7:26]
Mwenyezi Mungu anatubainisha kuwa amemteremshia mwanadamu mavazi/nguo za namna
mbili :
- Vazi la pambo hili ni kwa ajili ya kuupamba na kuusitiri utupu wake na
kumtofautisha na hayawani wengine.
- Vazi la ucha-Mungu hili ni kwa ajili ya kuipamba na kuisitiri nafsi yake na
kumfanya binadamu kamili mkamilifu wa utu na ubinadamu. Na hili ndilo vazi bora kama
alivyolisifia Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa sababu ni vazi hili ndilo humtoa mwanadamu
kutoka kwenye unyama na kumleta kwenye utu.
Mshairi wa kiarabu anaukiri ukweli huu, aliposema :
Ikiwa mtu hakuvaa vazi la ucha-mungu,
Huyo huwa utupu hata kama kavaa,
Na bora ya mambo ya mtu ni kumtii Mola wake,
Hapana kheri kwa mtu mwenye kumuasi Allah.
Na Mwenyezi Mungu anazidi kutuambia : "
NA AMEKUFANYIENI NGUO
ZINAZOKUKINGENI NA JOTO ( na baridi, na amekufanyieni) NGUO ZA CHUMA ZINAZOKUKINGENI
KATIKA VITA VYENU" [16:81]
Hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu anatubainishia aina kuu mbili za mavazi, kulingana na
majira ambazo ni :
- Mavazi ya joto (kiangazi)
- Mavazi ya baridi (masika)
Na pia mavazi maalum ya vita, haya ni pamoja na BULLET PROOF tuzionazo leo.
Tunasoma tena : "NA TUKAMFUNDISHA (Daudi) MATENGENEZO YA MAVAZI YA VITA KWA AJILI
YENU ILI YAKUHIFADHINI KATIKA MAPIGANO YENU JE MTAKUWA WANAOSHUKURU ?" [21:80]
Tunafahamikiwa kwamba kumbe sanaa ya utengenezaji wa mavazi ya vita ni sanaa
kongwe kabisa na mwanadamu wa kwanza kutengeneza mavazi ya vita ni Nabii Daudi
zimshukie amani-.
Naye mfasiri mkuu wa Qur-ani tukufu, Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie
anatufasiria aya hizo kwa kusema : "Kuleni, kunyweni, vaeni na toeni sadaka
bila ya israfu (kupita kiasi) wala maringo/fakhri".
Kadhalika, Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie ametufafanulia na
kutubainishia mavazi yanayojuzu/yanayofaa kuvaliwa na ambayo ni karaha. Kwa hivyo basi,
imempasa na kumlazimu muislamu kuzichunga na kuzifuata adabu/taratibu zifuatazo katika
suala zima la uvaaji wake :
- Mwanamume asivae kabisa nguo ya hariri kwa hali yeyote ile iwayo hata kama ni tai
au kitambaa cha kichwa. Hii ni amri ya Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie
aliposema : "Msivae hariri, kwani atakayeivaa duniani hatoivaa akhera" Bukhaariy
na Muslim. Na kauli yake Bwana Mtume il-hali akiwa ameishika hariri kwa mkono na dhahabu
mkono wa kushoto : "Hakika (vitu) viwili hivi ni haramu kwa wanamume wa umati
wangu" Abu Dawoud.
- Nguo yake isiwe ndefu sana kiasi cha kuburuza chini. Urefu wa nguo yake usizidi
kifundo cha mguu. Haya yanatokana na kauli ya Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie
- : "Mwenyezi Mungu hatomuangalia/ hatomtazama kwa jicho la rehema atakayeiburuza
nguo yake kwa maringo" Bukhariy na Muslim.
- Apendelee zaidi kuvaa nguo nyeupe pamoja na kuwa inafaa kuvaa nguo za rangi
nyingine. Hivyo ndivyo alivyotuelekeza Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie - :
"Vaeni nguo nyeupe kwani hizo ndizo twahara/safi na nzuri sana, na wakafinini maiti
wenu kwa nguo nyeupe (yaani washoneeni sanda nyeupe)" Nisaai na Al-Haakim. Na pia
imethibiti kwamba Bwana Mtume alivaa nguo ya kijani na alipiga kilemba cheusi.
- Mwanamke wa kiislamu avae vazi refu litakaloweza kusitiri hadi nyayo zake, aangushe
ushungi kiasi cha kusitiri shingo, na kifua chake. Akifanya hivyo atakuwa ameitii kauli ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo : "EWE MTUME! WAAMBIE WAKE ZAKO NA WANAWAKE WA
KIISLAMU WAJITEREMSHIE UZURI NGUO ZAO. KUFANYA HIVYO KUTAPELEKEA UPESI WAJULIKANE (kuwa ni
watu wa heshima ili) WASIUDHIWE .." [33:59]
Na kauli nyingine isemayo :
"
NA WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO NA WASIONYESHE MAPAMBO YAO ILA KWA
WAUME ZAOAU BABA ZAO
."
Na kwa kauli ya Mama Aysha Allah amuwie radhi- : "Mwenyezi Mungu
awarehemu wanawake muhaajirati wa mwanzo, Mwenyezi Mungu alipoteremsha : "
NA
WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO
" wakapasua maguo yao mazito na
kujitanda nayo" Bukhariy.
Na kwa kauli ya Ummu Salamah Allah amuwie radhi - : "Ilipoteremka :
"EWE MTUME! WAAMBIE WAKE ZAKO NA WANAWAKE WA KIISLAMU WAJITEREMSHIE UZURI NGUO ZAO
" Walitoka wanawake wa kiansari kama kwamba kuna kunguru vichwani mwao kutokana
na maguo waliyovaa na kujitanda" Muslim.
Hivi ndivyo wanavyotakiwa kuwa waislamu wa kweli, wakiamrishwa pale pale huamrika
na wakikatazwa hukatazika pasina kurudi nyuma.
- Mwanamume wa kiislamu asivae mavazi na mapambo ya kike na mwanamke muumini asivae
mavazi mavazi na mapambo ya kike na mwanamke muumini asivae mavazi na mapambo ya kiume.
Anasema Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie - : "Mwenyezi Mungu amemlaani
mwanamume anayevaa vazi la mwanamke na mwanamke avaaye vazi la mwanamume kama alivyolaani
wanamume wenye kujishabihisha na wanawake na wanawake wenye kujishabihisha na
wanamume" Muslim.
- Aanze kuvaa upande wa kulia wa nguo yake. Kama ni kanzu, shati, koti, gauni au
kizibao aanze kuvaa mkono wa kulia. Kama ni suruali basi aanze kuvaa mguu wa kulia. Haya
ni kwa mujibu wa kauli ya Mama Aysha Allah amuwie radhi Mtume wa Allah
Rehema na Amani zimshukie alikuwa akipenda kuanza kulia katika mambo yake
yote; katika uvaaji wake wa viatu, uchanaji wake nywele na kujitwahirisha kwake"
Bukhariy.
- Aseme anapovaa nguo mpya : Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndio mwenye sifa zote
uliyenivisha, nakuomba kheri yake na kheri iliyotengenezewa kwayo, na najilinda na shari
yake na shari iliyotengenezewa kwayo.
- Asivae nguo nyepesi yenye kuonesha ndani rangi ya mwili wake (transparent).
Kadhalika asivae nguo yenye kumbana sana kiasi cha kuchora ramani/finyango la mwili wake.
|